Meneja wa kundi hilo, Said Fella, amesema Yamoto Band watasafiri Jumatatu kuelekea nchini Afrika Kusini kushoot video hiyo.
“Wiki ijayo tunatarajia kufanya video mpya ya Yamoto Band na Godfather
atakuwa director,” Fella ameiambia Bongo5. “Hatuendi south kama kuiga
lakini madogo nao wanataka kwenda mbali zaidi.”
“Tunajaribu kuwapenyeza zaidi Afrika. Kwahiyo Diamond ndio kaongea na
Godfather na yeye ndo katoa hiyo ofa, hivyo hii ni ofa ya Nasib.
Tunakwenda Jumatatu, tunafanya video Jumanne na Jumatano kuna shughuli
tutaifanya tena,” alisema Fella.
0 comments :
Post a Comment