Baada ya kuingia studio kubwa za Universal kurekodi wimbo huo jana, Donald amesema wimbo huo utatoka wiki Ijayo.
Wakihojiwa kupitia kituo cha radio cha Kaya Fm 95.9 cha Afrika Kusini,
Donald akiwa na Diamond kwenye studio za radio hiyo amesema kuwa video
ya wimbo huo inatarajiwa kuanza kushutiwa Jumamosi hii.
Donald ameongeza kuwa sababu za kuamua kufanya kazi na Diamond ni
kutokana na ukubwa alionao, na baada ya kufanya utafiti wa msanii
anayeweza kumtambulisha vizuri Tanzania kwa kufanya naye kazi, bahati
hiyo ikamdondokea Diamond. Ameongeza kuwa amewahi kuombwa collabo na
wasanii wengi lakini hakuona kama wanaendana kama ilivyokuja kutokea kwa
Diamond.
“Hii
ni biashara ni muhimu kujua impact ya msanii unayetaka kufanya naye
kazi kabla hamjafanya, nilifanya utafiti wangu baada ya kusikia ukubwa
wa Diamond Platnumz, nikagundua huyu ndiye msanii nayeweza kuanza naye
safari yangu ya kujitangaza Afrika.”
Radio nyingine ya S.A waliyofanyiwa mahojiano juu ya collabo yao ni Metro Fm.
0 comments :
Post a Comment